ATHARI ZA BAWASIRI




 Bawasiri ni  vinyama au uvimbe unaotokea sehemu za haja kubwa. Nyama hizi huweza tokea kwa ndani au nje ya sehemu ya aja kubwa. Ugonjwa huu uwapata watoto hata na watu wazima.Ugonjwa huu uweza kuleta madhara mbalimbali katika mwili wa binadamu.  



NINI HUSABABISHA BAWASIRI.

Bawasiri husababishwa na changamoto mbalimbali za kiafya zifuatazo:
1.    Uzito au unene uliopitiliza .
2.    Kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
3.    Kukosa haja kubwa au kupata choo kigumu kwa mda mrefu.
4.    Kukaa chini kwa vipindi virefu.
5.    Kutumia vyoo vya kukaa. 
6.    Kuharisha kwa mda mrefu.
7.    Ukosefu wa nyuzinyuzi (fibers) kwenye mlo wa kila siku.
8.    Ujauzito.
9.    Kujizuia kwenda haja kubwa kwa wakati.
10.    Utu uzima.
  



DALILI ZA BAWASIRI.

1.    Muwasho sehemu za haja kubwa.
2.    Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa.

3.    Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa inaweza kutokea ndani au kuwa kwa nje kuzunguka mkundu. 4.    Haja kubwa kuwa na damu.
5.    Harufu mbaya na kali ya kinyesi wakati wa kujisaidia.
6.    Hali ya kujisikia kupata haja kubwa lakini hakitoki.
7.    Mumivu makali na kushindwa kukaa chini vizuri.
  




NINI KIFANYIKE KUZUIA UGONJWA WA BAWASIRI?

Bawasiri ni ugonjwa ambao unaweza zuilika kwa kufuata njia mbali mbali ili kujikinga. 
Maji ni mojawapo ya njia ya kuzuia ugonjwa huu kwa kunywa maji kwa wingi angalau glasi 8 hadi 10 kwa siku lakini pia kwa muda sahihi.
Kula mlo wenye nyuzi nyuzi za kutosha, kula matunda na vimiminika kwa wingi. Bila kusahau mazoezi kila siku.

 

  SULUHISHO LA BAWASIRI.

Ugonjwa huu mara nyingi unakuwa sio rahisi
i kugundulika, ila vilevile mara nyingi watu hugundua tatizo likiwa limeshakuwa kubwa. Na wanaogundua mara nyingi huishia kufanyiwa upasuaji ili kutoa vinyama/ uvimbe ambao unakuwepo sehemu ya haja kubwa. Lakini zipo tiba asilia ambayo zinaweza tumika kuepusha tatizo hili na kulitibu kama lipo..
Tiba asilia hizo husaidia kuongeza nyuzi nyuzi kwenye mlo, kuongeza vilainishi hivyo mtumiaji kupata haja kubwa laini na bila maumivu na vile vile zinasaidia kupunguza uvimbe au vinyama vyenyewe hivyo utumiaji endelevu hupelekea kupungua na hata kuisha kabisa kwa tatizo hili.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

CONSTIPATION

NATURAL TREATMENT OF HEMMORRHOIDS